Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Saad
Sura ya 38

Saad

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 31–33

إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِٱلْعَشِىِّ ٱلصَّـٰفِنَـٰتُ ٱلْجِيَادُ 31 فَقَالَ إِنِّىٓ أَحْبَبْتُ حُبَّ ٱلْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّى حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِٱلْحِجَابِ 32 رُدُّوهَا عَلَىَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًۢا بِٱلسُّوقِ وَٱلْأَعْنَاقِ 33

{31 - 33} Ndiyo maana walipoletwa mbele yake farasi hao waendao shoti, "wasimamao kidete" na wakaonekana kwa mwonekano mzuri wa kupendeza, hasa kwa wale wanaowahitaji, kama vile wafalme, na wakaendelea kuletwa mbele yake mpaka jua lilipozama kwenye upeo wa macho, kwa hivyo wakamshughulisha asiswali swala ya jioni na kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema akijutia hayo aliyoyafanya na akitaka kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa hayo yaliyomzuilia mbali kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na akautanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu mbele ya upendo wa wengineo: "Hakika mimi nimevipenda vitu vizuri" ambavyo ni mali kwa ujumla, na mahali hapa kilichokusudiwa ni farasi hao, "kuliko kumkumbuka Mola wangu Mlezi mpaka jua likapotelea kwenye upeo wa macho." "Warudisheni kwangu!" Basi wakawarudisha na "akaanza kuwapapasa miguu na shingo." Yaani, akaanza kuwachinja kwa kuwapiga kwa upanga wake kwenye miguu na shingo zao.