As-Saaffaat
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ 69 فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ 70 وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ 71 وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ 72 فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ 73
{69 - 73} Ni kana kwamba ilisemwa: Ni nini kilichowafikisha katika nyumba hii? Akasema: "Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao." Na hawakuzingatia yale waliyowaitia Mitume, wala yale ambayo vitabu viliwaonya dhidi yake, wala maneno ya washauri. Bali waliyapinga hayo kwa kusema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. "Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao" hawa wanaoongeleshwa, "wengi wa watu wa zamani," na ni wachache tu miongoni mwao ndio walioongoka. "Na Sisi hakika tuliwatumia waonyaji" ili wawaonye juu ya kukengeuka kwao na upotovu wao. "Basi, hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wale walioonywa." Mwisho wao ulikuwa maangamio, hizaya na fedheha. Basi na watahadhari watu hawa wasije wakaendelea katika upotofu wao, wakaja kupatwa na yale yale yaliyowapata hao.