Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saaffaat
Sura ya 37

As-Saaffaat

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 171–179

وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ 171 إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ 172 وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ 173 فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ 174 وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ 175 أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ 176 فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ 177 وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ 178 وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ 179

{171 - 179} Wala wasifikirie kuwa watakuwa washindi katika dunia hii. Bali tayari lilikwisha pita neno la Mwenyezi Mungu, ambalo haliwezi kupingwa wala hakuna anayeweza kulihalifu kwa waja wake waliotumwa na jeshi lake lililofaulu, kwamba watashinda wengine wote na kwamba wataokolewa na Mola wao Mlezi kwa nusura yenye nguvu ambayo kwayo wataweza kuisimamisha dini yao. Hii ni bishara kubwa kwa wale ambao wanasifika kwamba ni katika jeshi la Mwenyezi Mungu. Nao ni wale ambao hali zao zimenyooka na wakapigana vita dhidi ya wale ambao waliamrishwa kupigana nao, kwamba watashinda na watanusuriwa. Kisha akamwamrisha Mtume wake awaepuke wale waliokaidi na wakakataa kuikubali haki, na kwamba hakikubakia isipokuwa kungojea adhabu itakayowapata. Ndiyo maana akasema: "Na watazame, nao wataona" yule ambaye atapatwa na adhabu, kwani itawapata hao tu. "Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa." Kwa sababu itakuwa asubuhi ya shari, adhabu na kuangamizwa. Kisha akarudia amri ya kwamba aachane nao, na akawatishia kwamba watapatwa na adhabu.