As-Saaffaat
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ 114 وَنَجَّيْنَـٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ 115 وَنَصَرْنَـٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ 116 وَءَاتَيْنَـٰهُمَا ٱلْكِتَـٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ 117 وَهَدَيْنَـٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ 118 وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ 119 سَلَـٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ 120 إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ 121 إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ 122
{114 - 122} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja neema zake kwa waja wake na Mitume wake - Musa na Harun, na wana wa Imran kwa kuwapa Unabii, Utume, kulingania kwa Mwenyezi Mungu, kuwaokoa wao na watu wao kutoka kwa adui yao Firauni na kuwapa ushindi dhidi yao mpaka Mwenyezi Mungu akamzamisha ilhali wanatazama. Pia Mwenyezi Mungu akawateremshia Kitabu kinachobainisha ambacho ni Taurati, ambayo ndani yake kuna hukumu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaongoa kwenye njia iliyonyooka kwa kuwawekea dini yenye hukumu na sheria zilizonyooka zenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu, na akawawezesha kuifuata. "Na tukawaachia (sifa njema) katika watu waliokuja baadaye. Iwe salama kwa Musa na Haruni!" Yaani aliwafanya wasifiwe katika watakaokuja baadaye, kwa hivyo kusifiwa kwao katika waliotangulia ni kwingi zaidi. "Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini."