Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naml
Sura ya 27

An-Naml

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 2

هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ 2

{2} Hata hivyo, wengi wa walimwengu hawakunufaika nayo, na wapinzani wote hawakuongoka kwayo; ili kuilinda kutokana na wale ambao hawana heri ndani yao, wala kutengenea, wala utakaso mioyoni mwao. Lakini badala yake waliongoka kwayo wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachagua kwa imani na akaangaza mioyo yao kwayo na zikazifika hali zao za kisiri. Na ndiyo maana akasema, "Uwongofu na bishara kwa Waumini," yaani, yanawaongoa kufuata njia iliyonyooka, na kuwabainishia yale wanayopaswa kufuata au kuacha, na kuwabashiria thawabu za Mwenyezi Mungu zilizotokana na kuongoka kwenye njia hii.