Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 44

بَلْ مَتَّعْنَا هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَآ ۚ أَفَهُمُ ٱلْغَـٰلِبُونَ 44

{44} Kilichowawajibisha kuendelea na ukafiri wao na ushirikina ni kauli yake: "Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao." Yaani, tuliwaruzuku mali na watoto, na tukawarefushia maisha. Basi wakajishughulisha na kufurahishwa nayo, na wakapumbazwa nayo katika yale waliyo umbiwa, na maisha yao yakawa marefu, na nyoyo zao zikawa ngumu, ukawa mkubwa uasi wao; na ukafiri wao ukaongezeka. Ikiwa walivuta mazingatio yao kwa wale walio chini kulia na kushoto kwao katika ardhi; hawakupata chochote ila kuangamia, na hawakusikia ila sauti ya mwanamke akiomboleza, na walihisi tu karne nyingi za maangamizo mfululizo, na kifo kilikuwa kimeweka mitego kwenye kila njia - ili kuziteka roho. - Na ndiyo maana akasema: "Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake;" yaani, kwa kufa watu wake na kuangamizwa kwao kidogo kidogo mpaka Mwenyezi Mungu airithi ardhi na waliomo ndani yake, naye ndiye Mbora wa warithi. Kwa hivyo lau waliona hali hii; hawangedanganyika na kuendelea kama walivyokuwa. "Basi je, hao ni wenye kushinda" ambao kwa wasaa wao wanaweza kutoka katika uwezo wa Mwenyezi Mungu, na uwezo wao kujiepusha na kifo? Je, haya ndiyo maelezo yao mpaka wambadilishe kwa muda mrefu wa kubakia kwao? Au pindi atakapowajia mjumbe wa Mola wao, ili kuzichukua roho zao, watabaki wakinyenyekea na kudhalilika, bila hata kuonyesha upinzani japo mdogo?