Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 29

وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّىٓ إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّـٰلِمِينَ 29

{29} Na alipobainisha kwamba hawana haki yoyote katika uungu, wala hawastahiki kuabudiwa kwa namna yoyote ile kwa sifa alizowaelezea kwazo zinazolazimu hayo, akataja pia kwamba hawana fungu lolote, wala hata kwa kudai tu, na kwamba mwenye kusema miongoni mwao kwamba: Mimi ni mungu badala ya Mwenyezi Mungu - kwa njia ya kuchukulia tu kwamba hilo linawezekana na kukubali tu kujadili, "basi huyo tutamlipa malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo madhalimu." Na ni dhuluma gani kubwa zaidi kuliko kiumbe mpungufu, mwenye kumhitaji Mwenyezi Mungu kwa namna zote kudai kwamba anashirikiana na Mwenyezi Mungu katika sifa maalumu za uungu na umola!