Al-Anbiyaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
لَا يَسْبِقُونَهُۥ بِٱلْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِۦ يَعْمَلُونَ 27
{27} "Hawamtangulii kwa neno" lolote linalohusiana na uendeshaji wa ufalme wake mpaka Mwenyezi Mungu aseme mwenyewe, kwa sababu ya ukamilifu wa adabu yao na kujua kwao ukamilifu wa hekima yake na elimu yake. "Nao wanafanya amri zake" kwa namna gani atakavyowaamrisha. Na kwa namna gani atakavyowapangia, wao wanaifanya tu. Kwa hivyo hawamuasi hata kwa kiasi cha kupepesa jicho, na wala hawafanyi matendo yoyote yatakavyo matamanio yao bila ya kuamrishwa na Mwenyezi Mungu.