Al-Anbiyaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِىٓ إِلَيْهِ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعْبُدُونِ 25
{25} Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoelekeza kutajwa waliotangulia, na akaamrisha kuyarejelea waliyo nayo katika kubainisha suala hili, akabainisha kwa ubainisho kamili zaidi katika kauli yake, "Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu." Kwa hivyo, Mitume wote waliokutangulia wewe pamoja na vitabu vyao suala kuu zaidi la ujumbe wao na msingi wake ni kuamrisha kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika yeyote. Na kubainisha kwamba Yeye tu ndiye Mungu wa haki, anayeabudiwa, na kwamba kuabudu kisichokuwa Yeye ni batili.