Al-Anbiyaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
فَلَمَّآ أَحَسُّوا۟ بَأْسَنَآ إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ 12 لَا تَرْكُضُوا۟ وَٱرْجِعُوٓا۟ إِلَىٰ مَآ أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَـٰكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْـَٔلُونَ 13
{12 - 13} Na hakika hawa walioangamizwa wakati walipohisi adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake, na kukawafikia kuteremka kwake, hawakuweza kurudi, wala hawakuwa na njia yoyote ya kujinasua. Walipiga ardhi kwa miguu yao kwa majuto na wasiwasi na kuumwa sana kwa sababu ya yale waliyoyafanya. Kwa hivyo wakaambiwa kwa njia ya kuwakejeli, "Msikimbie! Na rejeeni kwenye yale yale mliyostareheshwa kwayo, na maskani zenu, ili mpate kuulizwa!" Yaani, hakutawafaa kukimbia na kujuta, lakini, ikiwa mna uwezo, basi rudini kwenye zile starehe zenu mlizostareheshwa kwazo, matamanio yenu, maskani zenu yaliyopambwa na dunia yenu ambayo iliwadanganya na kuwapumbaza mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ikaja. Basi bakieni humo kwa kuimarika, mfarijike kwa starehe zake, na mtulie katika maskani zenu kwa kutukuzwa, ili muweze kukusudiwa katika mambo yenu kama vile mlivyokuwa hapo zamani mkiulizwa katika matashi ya kidunia kama ilivyokuwa katika hali yenu ya hapo awali, lakini hilo haliwezekani kamwe!