Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sura ya 21

Al-Anbiyaa

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 112

قَـٰلَ رَبِّ ٱحْكُم بِٱلْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا ٱلرَّحْمَـٰنُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ 112

{112} "Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki;" Yaani, baina yetu na watu makafiri. Basi Mwenyezi Mungu akaijibu dua hii, na akahukumu baina yao katika dunia kabla ya Akhera kwa yale aliyowaadhibu nayo Mwenyezi Mungu makafiri katika vita vya Badr na vingine. "Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayoyazua." Yaani, tunamuomba Mola wetu, Mwingi wa Rehema, na tunamwomba msaada kwa yale mnayoyaeleza katika kusema kwenu: Tutawashinda, na Dini yenu itatoweka! Katika hili, hatujivutii nafsi zetu, wala hatutegemei walio karibu nasi na nguvu zetu, bali tunaomba msaada kwa Mwingi wa Rehema ambaye mkononi mwake kuna fungu la kila kiumbe, na tunataraji kwamba atakamilisha rehema tulizomuomba. Na akafanya hivyo, na sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu.