Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغْوِ فِىٓ أَيْمَـٰنِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ 225
{225} Yani (Mwenyezi Mungu) hawachukulii ubaya katika viapo vinavyopita tu juu ya ndimi zenu bila ya kuvikusudia, ambavyo mja anavisema bila ya yeye kuvikusudia wala kuchuma kwa moyo. Lakini vinapita tu kwenye ulimi wake, kama vile mtu kusema katika kuwasilisha maneno yake. “Hapana, wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu)” na “Ndiyo, wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu).” Na kama kiapo chake juu ya jambo lililopita analodhani kwama yeye ni mkweli. Na ama kuchukuliwa ubaya, huko kunakuwa kwa yale ambayo moyo umekusudia. Katika hili kuna ushahidi juu ya kuzingatia makusudio katika maneno, kama vile yanavyozingatiwa katika matendo. “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe.” Kwa anayetubia kwake “Mpole” kwa anayemuasi, kwa sababu hakumharakishia adhabu. Lakini alimfanyia upole na akasitiri, na akatupilia mbali pamoja na uwezo wake juu yake, kwamba yuko mbele yake.