Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱعْبُدُوا۟ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ 21
(21) Hii ni amri ya jumla kwa watu wote wenye amri ya jumla, ambayo ni ibada inayojumuisha kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na kuwacha makatazo yake, na kusadiki habari zake. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha lile alilowaumbia kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu alisema: "Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi". Kisha akaleta dalili ya ulazima wa kumuabudu Yeye peke yake, kwamba Yeye ndiye Mola wenu Mlezi ambaye amekuleeni kwa aina mbalimbali za neema. Alikuumbeni baada ya kutokuwepo, na akawaumba wale wa kabla yenu.