Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 207

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشْرِى نَفْسَهُ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ رَءُوفٌۢ بِٱلْعِبَادِ 207

{207} Hawa ndio waliowezeshwa, ambao waliziuza nafsi zao kwa bei nafuu na wakazitoa kwa kutafuta kumridhisha Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo yake. Basi wao walitoa thamani kumpa Mkwasi, Mwenye kulipa vikamilifu, Mpole kwa waja wake. Ambaye katika Upole wake na rehema zake ni kwamba aliwawezesha kufanya hayo, na akaahidi kulipa kwa ukamilifu, akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo.” Hadi mwisho wa Aya. Na katika Aya hii Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba waliziuza nafsi zao na wakazitoa. Na akajulisha kuhusu upole wake unaosababisha wao kupata walichoomba, na wakatoa walichokitaka. Basi usiulize baada ya haya yale yanayowapata kutoka kwa Mkarimu, na kile kinachowapata cha kufaulu na kuheshimiwa.