Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَٱقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَٱلْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ ٱلْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَـٰتِلُوهُمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَـٰتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَـٰتَلُوكُمْ فَٱقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْكَـٰفِرِينَ 191 فَإِنِ ٱنتَهَوْا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 192
{191-192} “Na waueni popote muwakutapo.” Hii ni amri ya kupigana nao popote wanakopatikana kila wakati na kila zama kupigana kwa kujilinda, na kupigana kwa kushambulia. Kisha akatoa katika ujumla huo kupigana nao “kwenye Msikiti Mtakatifu.” Na kwamba hilo haliruhusiki mpaka isipokuwa wao tu waanzishe kupigana, kwa hivyo, watapigana ili kuwalipa kuanzisha kwao vita. Na hilo litaendelea katika kila wakati mpaka waache ukafiri wao na wasilimu. Kwa maana, Mwenyezi Mungu atawakubalia toba pamoja na yale yaliyotokea kutoka kwao ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na ushirikina katika Msikiti Mtakatifu, na kumzuia Mtume na Waumini kuufikia. Na hili ni katika rehema na ukarimu wake kwa waja wake. Na kwa vile kupigana vita katika Msikiti Mtukufu kunaweza fikiriwa kuwa ni uharibifu katika ardhi hii tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa; uharibifu wa fitina hapo kwa ushirikina na kuizuia dini yake ni mbaya zaidi kuliko uharibifu wa kuua. Hivyo basi, hakuna ubaya wowote juu yenu - enyi Waislamu - katika kupigana nao. Aya hii inatumika juu ya msingi mashuhuri sana, ambao ni kufanya ovu dogo kati ya maovu mawili, ili kuzuia lililo juu zaidi ya mawili hayo.