Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 108

أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْـَٔلُوا۟ رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلْكُفْرَ بِٱلْإِيمَـٰنِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ 108

(108) Mwenyezi Mungu anawakataza Waumini au Mayahudi kumuuliza Mtume wao "kama alivyoulizwa Musa zamani."Na maana yake ni maswali ya ukaidi na upinzani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha muuliza Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni." Haya na mfano wake ndiyo yaliyokatazwa. Na ama swali la kutafuta mwongozo na kujifunza, basi hili ni jambo la kusifiwa, Mwenyezi Mungu ameamrisha hilo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu; "Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui." Na anawakubalia kwa hayo kama katika kauli yake: "Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari" na "Na wanakuuliza juu ya mayatima." na mfano wa hayo. Na kwa kuwa maswali yaliyokatazwa ni yenye kukashifiwa, ambayo huenda yakampelekea mwenyewe katika ukafiri, akasema: "Na anayebadilisha Imani kwa ukafiri, bila ya shaka huyo ameipotea njia iliyo sawa."