Al-Kahf
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَلَوْلَآ إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِ ۚ إِن تَرَنِ أَنَا۠ أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا 39
Kisha akajulisha kwamba neema za Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa imani na Uislamu, hata kama yeye ana uchache wa mali na watoto, hayo ndiyo neema ya uhakika, na kwamba chochote kisichokuwa hayo vinaweza kutoweka, na kumsababishia mtu adhabu na mateso. Akasema:
{39} Yaani, yule sahibu yake Muumini alimwambia yule rafiki yake kafiri: Hata kama unajifakhari mbele yangu kwa sababu ya wingi wa mali yako na watoto wako, na ukaniona mimi "nina mali kidogo na watoto kuliko wewe," basi hakika yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ya kubakia zaidi, na heri na wema unaotarajiwa kutoka kwake ni bora kuliko dunia yote ambayo wanashindana juu yake washindani.