Al-Hashr
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْمَلِكُ ٱلْقُدُّوسُ ٱلسَّلَـٰمُ ٱلْمُؤْمِنُ ٱلْمُهَيْمِنُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْجَبَّارُ ٱلْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ 23
{23} Kisha akarudia kutaja jumla ya uungu wake na upekee wake katika hilo, na kwamba yeye ndiye mmiliki wa falme zote. Ulimwengu wa juu na wa chini na wakazi wake wote ni waja wa Mweneyezi Mungu, wahitaji mno, na wanaendeshwa naye. “Mtakatifu, Mwenye salama.” Yaani, Mtakatifu, aliyesalimika na kila dosari, [balaa], na mapungufu, anayetukuzwa, anayeheshimiwa. Kwa sababu utakatifu unaonyesha kutakasika kwake kutokana na mapungufu yote na kutukuzwa kwa Mwenyezi Mungu katika sifa na utukufu wake. “Mtoaji wa amani” na pia ilisemekana kwamba maana yake ni mwenye kuwasadikisha Mitume na Manabii wake katika yale waliyokuja nayo kwa ishara zilizo wazi, na ushahidi wa kukata, na hoja zilizo wazi. “Mwenye nguvu” ambaye hashindwi wala hazuiliki. Bali Yeye ameshinda kila kitu, na kila kitu kiko chini yake. “Anayefanya analolitaka” ambaye aliwashinda waja wote, na viumbe vyote vikawa chini yake, ambaye anayewatia nguvu waliovunjika na kuwatajirisha masikini. “Mkubwa” mwenye ukubwa wote, na ukuu, ambaye ametakasika kutokana na kasoro, dhuluma na ukandamizaji. “Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo.” Huku ni kumtakasa kwa jumla kutokana na kila alichoelezewa kwacho na wale wanaomshirikisha na kumkaidi.