U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Suuradda 2

Al-Baqara

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 158

إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ ٱلْبَيْتَ أَوِ ٱعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ ٱللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ 158

(158) Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa, “hakika, vilima vya Safaa na Marwa” navyo ni vilima vinavyojulikana. “Ni katika alama za Mwenyezi Mungu,” yani alama za dhahiri za dini yake ambazo Mwenyezi Mungu amewafanya waja wake kumuabudu kwazo. Na ikiwa (vilima hivyo) ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu aliamrisha ziheshimiwe alama zake. Akasema, “na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” Kwa hivyo, jumla ya maandiko haya mawili yanaonyesha kuwa ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, na kwamba kuziheshimu alama zake ni katika uchamungu wa nyoyo. Nao uchamungu ni wajibu kwa kila aliyeamrishwa. Na hilo linaashiria kuwa kwenda kati ya viwili hivyo, (Sa’ayi) ni faradhi ya lazima katika Hijja na Umra kama wengi wa wanazuoni wanavyoona. Na hadithi za Nabii ziliashiria hivyo. Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – aliifanya (hiyo Sa’ayi), na akasema: “Chukueni ibada zenu kutoka kwangu”. “Basi, anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka.” Hili ni ili kuondoa dhana potofu ya yule aliyedhani vibaya na akaona ubaya miongoni mwa Waislamu kuzunguka baina yake kwa sababu, walikuwa katika siku za ujinga masanamu yalikuwa yakiabudiwa hapo. Basi Mwenyezi Mungu akakanusha ubaya ili kuzuia dhana hiyo potofu, siyo kwa sababu siyo lazima. Na kuzuilia huo ubaya kwa mwenye kuvizunguka katika Hijja au Umra kunaashiria kuwa mtu hawezi kujitolea kuvizunguka hivyo peke yake isipokuwa kwa kuunganisha hilo na Hijja au Umra. Tofauti na kuizunguka Nyumba, imeekwa kama sheria pamoja na Umra na Hija, nayo pia ibada kivyake. Ama kufanya Sa’ayi, kusimama Arafa na Muzdalifah, na kuipiga Jamarat kwa vijiwe, hayo yanafuata matendo ya Hijja. Na lau kuwa yatafanywa bila ya kuyaunga na matendo ya Hijja, basi yanakuwa uzushi (Bid'a). Kwa sababu, uzushi ni aina mbili: Aina ya kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa ibada ambayo hakuiweka katika sharia kabisa. Na aina nyingine ni kumuabudu Yeye kwa ibada aliyoiweka katika sheria kwa njia maalumu, lakini ikafanywa kwa njia isiyokuwa hiyo. Na hii ni katika aina hii. Na kauli yake, "na anayejitendea mwenyewe." Mwenye kutenda kitendo cha utiifu akikusudia kwayo Mwenyezi Mungu Mtukufu, "heri" kama vile hijja, umra, kuizunguka Al-Kaba, swala, saumu na mengineyo, basi hilo ni bora kwake. Na hili linaashiria kwamba kila mja anavyoongeza kumtii Mwenyezi Mungu, ndivyo heri yake inavyoongezeka. Na ukamilifu wake, na daraja yake kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kuongezeka kwa imani yake. Na aliiashiria kuzuilia kujitolea katika heri kuwa mwenye kujitolea kwa kufanya uzushi ambao Mwenyezi Mungu hakuuweka kama sheria wala Mtume wake. Kwamba hilo hatapata isipokuwa taabu tu, na wala siyo heri kwake. Bali huenda ikawa shari kwake ikiwa anaifanya kuwa ibada pamoja na kujua kuwa siyo katika sheria kuifanya, "basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mwenye elimu." Ash-Shakir na Ash-Shakur ni katika majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anakubali kutoka kwa waja wake matendo madogo. Na anawalipa kwayo malipo makubwa, ambaye mja wake anapofanya maamrisho yake na akatekeleza ya kumtii, yeye humsaidia katika hilo. Na anamsifu, na kumlipa nuru moyo wake, na imani, na wasaa, na katika mwili wake nguvu na nashati, na katika hali zake zote kuongezeka kwa baraka na kukua. Na katika matendo yake kuongezeka kuwezeshwa, kisha baada ya hayo atayaendea malipo ya baadaye kwa Mola wake Mlezi kwa ukamilifu, nyingi hali ya kuwa havipungukiwi vitu hivyo. Na katika kumshukuru kwake mja wake ni kwamba mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atampa kilicho bora kuliko hicho. Na mwenye kumkaribia kwa shubiri moja, basi yeye atamkaribia dhiraa moja. Na wenye kumkaribia kwa dhiraa moja, yeye atamkaribia kwa mkono mmoja. Na mwenye kumjia kwa kutembea, yeye atamjia kwa hatua za haraka. Na mwenye kuamiliana naye, atapata faida mizidisho mingi. Na pamoja na kwamba yeye ni mwenye kushukuru, lakini anajua ni nani anayestahiki ujira kamili kulingana na nia yake, imani, na uchamungu wake, kutokana na yule asiyekuwa hivyo. Anayajua matendo ya waja, basi Yeye hayapotezi, bali wanayakuta ni mengi zaidi kuliko yalivyokuwa kulingana na nia zao ambazo alizijua Mwenye elimu. Mwenye hekima.