Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Surah 6

Al-An'aam

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 99

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَخْرَجْنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَىْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ ٱلنَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّـٰتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَٱلزَّيْتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَـٰبِهٍ ۗ ٱنظُرُوٓا۟ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثْمَرَ وَيَنْعِهِۦٓ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكُمْ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ 99

{99} Na hii ni miongoni mwa neema zake kubwa zaidi ambazo viumbe vyote wanazihitaji sana miongoni mwa wanadamu na wengineo. Nayo ni kwamba aliteremsha maji kutoka mbinguni kwa mfululizo wakati watu wanapoyahitaji. Kisha Mwenyezi Mungu akaoteshea kwayo kila kitu miongoni mwa vile wanavyovila watu na mifugo. Kwa hivyo viumbe vikalia kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na wakawa na wasaa kwa riziki yake, na wakafurahia kwa sababu ya ihsani yake, na wakaondokewa na kiangazi, na kukata tamaa, na ukame. Kwa hivyo nyoyo zao zikafurahi, na nyuso zikang’aa, na waja wakapata katika rehema ya Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, yale ambayo wanafurahi kwayo na wanakula, jambo ambalo linawasababishia kufanya juhudi zao katika kumshukuru Yule aliyewapa neema hizo, na kumuabudu Yeye, na kurudi kwake, na kumpenda. Na Alipotaja ujumla wa aina za vile vinavyomea kwa maji miongoni mwa aina mbalimbali za miti na mimea, Akataja mazao na mitende kwa sababu ya wingi wa manufaa yake na kuwa ni chakula kikuu cha wengi wa watu. Kwa hivyo akasema, "Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani;" yaani, kutokana na mimea hiyo ya kijani tunatoa "nafaka zilizopandana," baadhi yake zikiwa juu ya nyingine zake, kama vile ngano, na shayiri, na mahindi, na mchele na aina nyinginezo za mazao. Na katika kueleza kwake kuwa zinapandana kuna ishara kwamba nafaka zake ni nyingi, na zote zimetokana na kitu kimoja, wala hazichanganyikani, bali ni nafaka zilizo mbalimbali lakini zenye asili moja. Na kuna ishara ya wingi wake, na wingi wa kubaki kwake na mapato yake, ili msingi wa mbegu hii ubaki, na mengi yabaki ya kula na kuhifadhi. "Na kutokana na mitende" Mwenyezi Mungu alitoa "katika makole yake;" nayo ganda la mtende kabla ya shada kutoka humo. Kisha yanatoka kutoka katika ganda hilo "mashada yaliyo karibu" yani, yaliyokaribu ambayo ni rahisi kuyachuma, yanayoinama karibu sana na mwenye kuyataka kiasi kwamba siyo vigumu kuyachuma kutoka kwenye mitende, hata kama ni mirefu. Kwa maana yana karab (yani sehemu ya mwanzo kabisa katika tawi la mtende) na vipandio ambavyo vinafanya kuwa rahisi kuipanda. "Na" Yeye Mtukufu Akatoa kwa maji haya "mabustani ya mizabibu, na mizaituni, na mikomamanga." Basi hii ni miongoni mwa miti yenye manufaa mengi, na thamani kubwa. Na ndiyo maana mwenyezi Mungu akayataja kwa njia maalumu baada ya kuitaja miti yote na mimea kwa ujumla. Na kauli yake. " yanayofanana na yasiyofanana;" inawezekana kuwa inarudi kwa makomamanga na mazaituni, yaani inayofanana katika mti wake na majani yake, lakini matunda yake hayafanani. Na inawezekana kwamba hilo linarudi kwa miti yote na matunda, na kwamba baadhi yake inafanana yenyewe kwa yenyewe, na inakaribiana katika baadhi ya sifa zake. Na baadhi yake haifanani na mingineyo. Na yote wananufaika kwayo waja, na wanayala matunda yake, na wanayala kama chakula kikuu, na wanapata mazingatio. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akaamrisha kuzingatia katika hayo, kwa hivyo akasema: "Angalieni," kuangalia kwa kutafakari na kuzingatia "matunda yake." Yaani, ya miti yote, hasa mitende, "yanapozaa na yakaiva;" yaani yatazameni wakati wa kuchipuka kwake, na wakati wa kukomaa kwake, na kuiva kwake. Kwani katika hayo kuna mazingatio, na Aya mbalimbali zinazotumiwa kuwa ushahidi juu ya rehema ya Mwenyezi Mungu, na upana wa ihsani yake, na kuwepo Kwake, na ukamilifu wa uwezo Wake, na uangalizi Wake mzuri kwa waja Wake. Hata hivyo, si kila mmoja anayezingatia na anatafakari; na si kila mwenye kutafakari akaitambua maana iliyokusudiwa. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akafungia kunufaika kwa Aya hizi kwa Waumini tu, kwa hivyo akasema, "Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini." Kwa sababu Waumini wanabebwa na imani waliyo nayo kufanya kulingana na matakwa yake, na mahitaji yake ambayo miongoni mwake ni kutafakari katika Aya za mwenyezi Mungu na kutoa kutoka kwayo yale yanayokusudiwa kwayo, na yale ambayo hayo yanayaashiria kiakili, na kiamaumbile ya asili, na kisheria.