At-Tawba
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَرِحَ ٱلْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَـٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓا۟ أَن يُجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُوا۟ لَا تَنفِرُوا۟ فِى ٱلْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا۟ يَفْقَهُونَ 81
{81} Yeye Mtukufu anasema akibainisha kujifahiri kwa wanafiki kuhusu kusalia kwao nyuma na kutojali kwao hilo, jambo linaloashiria kutoamini kwao na kuchagua kwao ukafiri kuliko imani: "Walifurahi walioachwa nyuma kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu" na hiki ni kiasi cha ziada juu ya kusalia nyuma tu. Kwani, huku ni kusalia nyuma kulikoharamishwa na kuongezea kuridhia kutenda maasia na kujifahirisha juu yake. "Na wakachukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu." Na haya ni kinyume na Waumini ambao wakisalia nyuma hata kwa sababu ya udhuru, walihuzunika huzuni mkubwa sana, na wanapenda kwamba wafanye jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya imani iliyo ndani ya mioyo yao, na wanatarajia katika fadhila za Mwenyezi Mungu, na ihsani yake, haki, na wema wake, na neema yake. "Na wakasema;" yaani,wanafiki: "Msitoke kwenda katika joto! " Yaani walisema, hakika kutoka kwenda ni kugumu juu yetu kwa sababu ya joto. Kwa hivyo wakatanguliza raha fupi ya kwisha kuliko raha ya milele kamilifu, na wakatahadharisha dhidi ya joto ambalo linakingwa na vivuli na linaodoshwa na kuingia kwa asubuhi na jioni badala ya joto kali ambalo haliwezi kupimwa kiwango chake. Nao ni Moto uwakao vikali, na ndiyo maana akasema, "Sema: Moto wa Jahannamu una joto kubwa zaidi, laiti wangelikuwa wanafahamu!"