Al-Mumtahana
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلْمُؤْمِنَـٰتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِٱللَّهِ شَيْـًٔا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَـٰدَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَـٰنٍ يَفْتَرِينَهُۥ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِى مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَٱسْتَغْفِرْ لَهُنَّ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 12
{12} Masharti haya yaliyotajwa katika Aya hii yanaitwa kiapo cha utii cha wanawake, ambao walikuwa wakipeana ahadi ya utii juu ya kutekeleza majukumu ya wajibu wanayoshiriki ndani yake wanaume na wanawake wakati wote. Ama wanaume, yale yanayowalazimu yanatofautiana kulingana na hali zao, daraja zao, na yale yanayowalazimu wao tu. Basi Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akitekeleza yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, alikuwa wanawake wanapomjia, wakimpa kiapo chao cha utii na kushika sawasawa masharti haya, anawachukulia viapo hivyo vya na kuliwaza nyoyo zao, na kuwaombea Mwenyezi Mungu msamaha kwa mapungufu yao, na kuwajumuisha miongoni mwa Waumini, “kwa sharti kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote,” bali watampwekesha Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada. “Wala hawatawauwa watoto wao” kama walivyokuwa wakifanya wanawake wajinga wa zama za kabla ya Uislamu. “Wala hawatazini” ilivyokuwa ikifanywa sana na wazinzi wa kike na kufanya urafiki wa kimapenzi na wanaume wasiokuwa waume zao. “Wala hawataleta uzushi wanaouzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao” katika kila hali, sawa uwe unahusiana na waume zao au unahusiana na mtu mwingine “wala hawatakuasi katika jambo jema.” Yaani, hawatakuasi katika kila amri unayowaamrisha. Kwa sababu amri yako haiwezi kuwa ila kwa wema. Na katika hili ni utiifu wao kwako katika kukataza kwako kuomboleza kwa sauti kubwa, kurarua mifuko ya nguo zao (katika kuomboleza), kujikwaruza uso, na kuomba dua za zama za kabla ya Uislamu. “Basi peana nao ahadi” ikiwa watashikamana na yote yaliyotajwa, “na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu” katika yale waliyozembea, na kwa ajili ya kuwafurahisha mawazo yao. “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira” kwa wanaoasi na ni mwenye kuwafanyia wema wafanyao dhambi na wakatubu. “Mwenye kurehemu mno.” Ambaye rehema zake zimekienea kila kitu na wema wake umekijumuisha kila kiumbe.