Al-Maaida
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَلَوْ كَانُوا۟ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلنَّبِىِّ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا ٱتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَآءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَـٰسِقُونَ 81
{81} "Na lau wangelikuwa wanamwamini Mwenyezi Mungu, na Nabii huyu, na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao kuwa marafiki wandani." Kwa maana, kumwamini Mwenyezi Mungu, na Nabii, na yale yaliyoteremshwa kwake yanamlazimu mja kumfanya Mola wake Mlezi kuwa rafiki mwandani. Na kuwa rafiki mwandani wa marafiki zake, na kuwafanyia uadui mwenye kumkufuru, na akamfanyia uadui, na akaharakisha katika kumuasi. Basi Sharti la kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa rafiki mwandani na kumwamini Yeye ni kwamba asiwafanye maadui wa Mwenyezi Mungu kuwa marafiki wake wandani. Na hawa sharti hili halikupatikana kwao, basi likaashiria kutokuwepo kila kilichowekewa sharti hilo. "Lakini wengi miongoni mwao ni wapitao mipaka." Yaani, wanatoka nje ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kumwamini Yeye na Manabii. Na katika kutoka kwao nje ya mipaka ni kuwafanya maadui wa Mwenyezi Mungu kuwa marafiki wao wandani.