Al-Maaida
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا۟ عَلَيْهِمْ ۖ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ 34
{34} "Isipokuwa wale waliotubia kabla hamjawatia nguvuni; yaani, miongoni mwa wapiganaji hawa. "Basi jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani, anamwachila yale yaliyokuwa ya Mwenyezi Mungu kama vile ulazima wa kuuawa, na kusulubiwa, na kukatwa mikono na miguu, na kufukuzwa kutoka katika nchi, na pia katika haki ya mwanadamu ikiwa mpiganaji huyo alikuwa kafiri kisha akasilimu. Lakini ikiwa mpiganaji huyo ni Mwislamu, basi haki ya binadamu haianguki kwake kama vile kuua na kuchukua mali. Na maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja iliashiria kuwa toba ya mpiganaji baada ya kutiwa nguvuni haifanyi chochote katika adhabu kuanguka. Na Hekima katika hayo iko wazi. Na ikiwa toba kabla ya kumtia nguvuni inazuia kumtekelezea adhabu maalum ya kisheria katika wale wanaompiga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi nyinginezo miongoni mwa adhabu maalum za kisheria akitubia mwenye kuzifanya kabla ya kutiwa nguvuni zinafaa zaidi kusamehewa.