Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sūrah 4

An-Nisaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 59

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ وَأُو۟لِى ٱلْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَـٰزَعْتُمْ فِى شَىْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا 59

{59} Kisha akaamrisha kumtii Yeye na Mtume wake. Na hilo ni kwa kufuata amri zao za wajibu na za kupenedekezwa, na kujiepusha na makatazo yao. Na akaamrisha kuwatii wenye mamlaka. Nao ni wale wanaowatawala watu miongoni mwa viongozi, na mahakimu, na wale wanaotoa Fatwa (hukumu ya kisheria kwa jambo fulani). Kwani watu jambo la dini la watu haliwezi kunyooka isipokuwa kwa kuwatii na kuwafuata, ili kumtii Mwenyezi Mungu na kutaka yale yaliyo kwake, lakini kwa sharti kwamba wasiamrishe kumuasi Mwenyezi Mungu. Na ikiwa wataamrisha hivyo, basi hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Na huenda hii ndiyo siri katika kufuta kitenzi wakati wa kuamrisha kuwatii na kukitaja pamoja na kumtii Mtume. Kwani, Mtume haamrishi isipokuwa kumtii Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumtii, basi atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu. Na ama wenye mamlaka, sharti la amri ya kuwatii ni kwamba isiwe ya maasia. Kisha akaamrisha kurudisha kila wanachozozana watu ndani yake miongoni mwa misingi ya dini, na matawi yake kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume. Yani kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake. Kwani, ndani ya viwili hivyo kuna hukumu ya kukata katika masuala yote yenye utata. Ima ya waziwazi yake, au ya ujumla yake, au kwa kuashiria, au kutanabahisha, au kwa maana ya kinyume, au ujumla wa maana ambayo inapimwa juu yake chenye kufanana nao. Kwa sababu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake juu yake kuna mjengo wa Dini, na wala imani hainyooki isipokuwa kwa viwili hivyo. Kwa hivyo, kurudisha kwa viwili hivyo ni sharti katika imani. Na ndiyo maana akasema, "ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho." Basi, hilo likaashiria ya kwamba asiyerudisha kwa viwili hivyo masuala yenye mzozo, basi yeye si Muumini kihakika, bali anaamini Taghut. Kama ilivyotajwa katika aya inayoifuata, "hilo" yani kurudisha kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. "Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema." Kwa maana hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo hukumu iliyo bora zaidi, na ya uadilifu zaidi, na nzuri zaidi kwa watu katika mambo ya dini yao, na dunia yao na mwisho wao.