Az-Zumar
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ ٱجْتَنَبُوا۟ ٱلطَّـٰغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ لَهُمُ ٱلْبُشْرَىٰ ۚ فَبَشِّرْ عِبَادِ 17
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja hali ya wahalifu,akataja hali ya waliotubu na malipo yao, akasema: "Na wale wanaojiepusha kuabudu Taghuti," yaani, chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Hii ni mbinu nzuri zaidi ya kuondoa kitu katika vinginevyo ambayo Yeye Mwenye hekima na ajuaye zaidi alitumia hapa. Kwani wale waliojiepusha kuabudu Taghuti ndio wanaofaa kusifiwa peke yao. "Na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu" kwa kumuabudu na kumkusudia Yeye tu katika Dini. Basi dhamira zao zikatoka katika kuabudu masanamu na kwenda katika kumwabudu Mfalme Mjuzi zaidi, na kutoka katika ushirikina na maasia na kuingia katika kumpwekesha na kumtii. "Watapata bishara njema," ambayo kiwango chake hakiwezi kupimwa wala hajui jinsi ilivyo haswa isipokuwa yule aliyewatukuza kwayo. Hili linajumuisha bishara njema katika maisha ya dunia kwa kupewa sifa njema, maoni mazuri na kutunzwa na Mwenyezi Mungu ambayo kwayo wanaona kuwa anakusudia kuwatukuza duniani na akhera. Na pia wanayo bishara njema katika akhera wakati wa kufa, katika kaburi na katika siku ya Kiyama. Na hitimisho la bishara yao njema ni yale ambayo Mola wao Mlezi, Mkarimu atawabashiria ya radhi zake za kuendelea juu yao, wema wake, ihsani yake na kupata amani yake Peponi.