As-Saaffaat
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَنَظَرَ نَظْرَةً فِى ٱلنُّجُومِ 88 فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ 89 فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ 90 فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ 91 مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ 92 فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ 93
{88 - 93} Basi yeye, amani iwe juu yake, akataka kuyavunja masanamu yao na aweze kufanya hivyo. Kwa hivyo, akaichukua fursa hiyo ilhali hawajui walipokuwa wamekwenda kwenye moja ya sikukuu zao, naye pia akatoka pamoja nao. "Kisha akapiga jicho kutazama nyota. Akasema: 'Hakika mimi ni mgonjwa!'" Imesimuliwa katika hadithi sahihi kuwa: “Ibrahim, amani iwe juu yake, hakusema uongo ila uongo tatu: kauli yake: 'Mimi ni mgonjwa,' na kauli yake: 'Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao,' na kauli yake kuhusu mkewe: 'Yeye ni dada yangu.'" Makusudio ya kufanya hivyo ni ili asalie nyuma yao aweze kukamilisha njama yake dhidi ya miungu yao hiyo. Ndiyo maana "wakamwacha, wakampa kisogo wakienda." Basi alipoipata nafasi hiyo, "akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia" kwa njia ya kejeli "Mbona hamli? Kwa nini hamuongei?" Yaani, vipi inafaa kuabudiwa ilhali ni mipungufu hata kuliko wanyama wanaokula na kuzungumza, na hali hiyo ni vitu visivyo na uhai ambavyo havili wala havisemi? "Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia." Na akaivunja vipande vipande ila kubwa lao, ili wao walirudie.