Ash-Shu'araa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَأُلْقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ 46 قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ 47 رَبِّ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ 48
{46-48} Wakati wachawi hao walipoona ishara hizi kubwa, wakawa na yakini baada ya kujua kwamba hilo halikuwa uchawi, lakini lilikuwa ishara miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu na muujiza ambao ulijulisha ukweli wa Musa na usahihi wa yale aliyokuja nayo. "Hapo wachawi hao walipinduka wakasujudu" kwa ajili ya Mola wao Mlezi. "Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote." Mola Mlezi wa Musa na Harun," na batili yao hiyo ikafutiliwa mbali katika mkusanyiko huo, na wakubwa wake wakakiri ubatili wake, na haki ikawa wazi na ikadhihirika hadi watazamaji wakaiona kwa macho yao.