Ash-Shu'araa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَـٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ 49 قَالُوا۟ لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ 50 إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَـٰيَـٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلْمُؤْمِنِينَ 51
{49 - 51} Lakini Firauni akakataa isipokuwa kuendelea kuwa na kiburi, upotovu na kuendelea katika upotofu wake na ukaidi. Akawaambia wachawi hao, "Je, mmemuamini kabla ya kuwaruhusu?" Huku akishangaa na kushangaza kaumu yake juu ya ujasiri wao wa kuchukua hatua ya kuamini bila idhini yake na kutafuta ushauri wake. "Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliyewafunza uchawi." Anasema hivyo, ilhali yeye ndiye aliyewakusanya wachawi hao na waheshimiwa wake ambao walimshauri kuwakusanya kutoka mijini mwao, na walikwisha jua kwamba hawakuwahi kukutana na Musa wala hata kumwona kabla ya hapo, na kwamba walifanya uchawi wa kuwachanganya watazamaji na kuwatisha, lakini pamoja na hayo, akaeneza kauli hii dhidi yao hata wao wenyewe walijua kwamba ni kauli batili. Kwa hivyo, halitakuwa jambo geni kwa watu wa akili hizi kutoamini haki hii iliyo wazi na ishara hizi za ajabu; kwa sababu ikiwa Firauni angewaambia chochote kile kwamba hicho ni kinyume na uhakika wake, wao wangemuona tu kuwa ni mkweli. Kisha akawatishia wachawi hao, na akasema, "Nitakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha;" yaani, mkono wa kulia na mguu wa kushoto; kama anavyofanyiwa mwenye kufanya uharibifu katika ardhi. "Na nitawasulubisha misalabani nyote" ili mdhalilike na mdunike. Basi wachawi hao wakasema walipopata utamu wa imani na wakaonja raha yake, "Haidhuru" kwani hatujali hicho unachotuhofisha kwacho; "kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi ili atatusamehe makosa yetu" ya ukafiri, uchawi na mengineyo; "kwa kuwa tumekuwa wa kwanza wa Waumini" waliomuamini Musa katika majeshi hawa. Basi Mwenyezi Mungu akawafanya wawe thabiti na wenye subira. Na inawezekana kwamba Firauni alifanya kile alichowatishia kufanya kwa sababu ya mamlaka yake na uwezo wake wakati huo, na inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu alimzuia kutia katika hayo.