Al-Anbiyaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَوْمَ نَطْوِى ٱلسَّمَآءَ كَطَىِّ ٱلسِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَآ أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُۥ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا فَـٰعِلِينَ 104
{104} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba Siku ya Kiyama atazikunja mbingu kwa ukubwa na upana wake, kama mwandishi anavyokunja kitabu; yaani, karatasi ambayo imeandikwa. Kisha nyota zake zitatawanyika, jua lake na mwezi wake vitakuwa mviringo, na vitatoweka kutoka mahali pake. "Kama tulivyoanza umbo la mwanzo tutalirudisha tena;" yaani, kurudi kwetu katika uumbaji ni kama mwanzo wetu wa kuwaumba. Kama vile tulivyowaumba wao wakiwa si kitu; hivyo ndivyo tutakavyowarudisha baada ya kufa kwao. "Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao:" Tutatekeleza tuliyoahidi, kwa sababu ya uweza wake mkamilifu, na kwamba hakuna kitu kinachozuiliwa kwake.