Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَلَمَّا جَآءَهُمْ كِتَـٰبٌ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا۟ مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُوا۟ كَفَرُوا۟ بِهِۦ ۚ فَلَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ 89 بِئْسَمَا ٱشْتَرَوْا۟ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا۟ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ 90
(89-90) Yani "Na kilipowajia [Kitabu]" kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mikono ya mbora wa viumbe na mwisho wa Manabii, kinachojumuisha kusadikisha yale waliyo nayo katika Taurati. Na walikwishamjua, na wakawa na yakini juu yake kiasi kwamba vita vilipokuwa vinatokea baina yao na washirikina katika zama za kabla ya Uislamu, wangetafuta msaada kupitia Nabii huyu. Na wangewaonya kuwa atatokea, na kwamba watapigana na washirikina pamoja naye. Basi kilipowajia kitabu hiki na Nabii huyo ambaye walimjua; walimkufuru kwa dhuluma na husuda kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia katika fadhila zake amtakaye katika waja wake. Basi Mwenyezi Mungu akawalaani na akawakasirikia ghadhabu baada ya ghadhabu, kwa sababu ya ukafiri wao mwingi na mfuatano wa shaka yao na ushirikina wao. Na huko Akhera wana adhabu idhalilishayo, yani adhabu chungu yenye kuumiza. Nayo ni kuingia Jahiim na kukosa neema ya milele. Basi hali mbaya mno ni hali yao. Na ni kibaya mno walichobadilishana na kubadilisha badala ya kumwamini Mwenyezi Mungu, na Vitabu vyake na Mitume Wake, wakakumkufuru Yeye na Vitabu vyake na Mitume wake pamoja na kujua kwao na yakini yao. Basi likawa ni kubwa mno la kuwaadhibu kwa sababu yake.