انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · العلق
السورة ٩٦

العلق

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣–٥

ٱقْرَأْ وَرَبُّكَ ٱلْأَكْرَمُ ٣ ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلْقَلَمِ ٤ عَلَّمَ ٱلْإِنسَـٰنَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ٥

{3 - 5} Kisha akasema: "Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!" Yaani, ana sifa nyingi za upana, ni mwingi wa ukarimu na hisani, na ni Mpaji kwa wingi, ambaye katika ukarimu wake ni kwamba alifundisha aina mbalimbali za elimu, na "Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui." Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtoa tumboni mwa mama yake ilhali hajui chochote, na akampa uwezo wa kusikia, kuona, na ufahamu wa moyo, na akamwepesishia njia za elimu. Basi akamfundisha Qur-ani, akamfundisha hekima, na akamfundisha kwa kalamu, [ambayo kwayo zinahifadhiwa elimu] na haki zinawekwa sawasawa, na zinakuwa ni Mitume kwa watu zinazowakilisha mahali pa kuzungumza kwao. Basi sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu ambaye amewajaalia neema hizi waja wake, ambazo hawawezi kuzilipa wala kushukuru, kisha akawaruzuku mali na riziki nyingi.