الشرح
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا ٥ إِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا ٦
{5 - 6} Na kauli yake: "Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. Hakika pamoja na uzito upo wepesi." Hii ni bishara kubwa kwamba kila inapopatikana dhiki na shida, basi urahisi unaambatana nayo na kuwa pamoja nayo, kiasi kwamba hata ikiwa uzito utaingia kwenye shimo la mjusi, basi wepesi ungeuingilia humo na kuutoa nje. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja," na kama Nabii - rehema na amani zimshukie -alivyosema: "Hakika pamoja na dhiki kuna faraja, na hakika pamoja na dhiki kuna wepesi." Neno uzito katika Aya hizi mbili limekuja kama nomino maalumu ili kuashiria kwamba ni mmoja, nalo neno wepesi limetumika katika hali ya nomino ya kawaida ili kuashiria kwamba wepesi hujirudiarudia. Kwa hivyo, uzito mmoja hauwezi kushinda wepesi mbili. Na pia matumizi ya herufi alif na lam katika neno uzito kwa Kiarabu, yenye maana ya ujumla, yanaashiria kwamba kila uzito hata ukiwa mgumu kiasi gani, lazima mwishoni mwake kuna wepesi.