الليل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَٱتَّقَىٰ ٥ وَصَدَّقَ بِٱلْحُسْنَىٰ ٦ فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْيُسْرَىٰ ٧
{5 - 7} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliwapambanua watendaji matendo na akaelezea vitendo vyao, akisema: "Ama mwenye kutoa" yale aliyoyaamrisha miongoni mwa ibaada za kimali, kama vile zaka, matumizi ya nyumbani, kafara, sadaka na kutoa sadaka kwa ajili ya mambo mengine ya heri, na vile vile ibada za kimwili, kama vile kuswali, kufunga saumu na mengineyo, na vile vile ibada zinazojumuisha hayo kama vile Hija, Umra, na zinginezo. "na akamcha Mungu" katika yale aliyokatazwa ya haramu na maasia ya aina mbalimbali. "Na akasadiki lililo jema" yaani hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, na yale inayoashiria imani hii ya itikadi zote za kidini, na yale yanayoambatana nayo ya malipo ya kiakhera. "Tutamsahilishia yawe mepesi." Yaani, tutamsahilishia mambo yake kwa kufikia yaliyo ya heri na kuacha maovu. Kwa sababu alifanya visababu vya kurahisishiwa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamfanyia rahisi.