انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٥

سَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمْ إِذَا ٱنقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ ٩٥

{95} Na jua kwamba mwenye kufanya mabaya, mwenye kufanya dhambi ana hali tatu: Ima ikubalike kauli yake na udhuru wake kwa nje na kwa ndani, na asamehewe kwa namna kwamba anabaki kama kwamba hakufanya dhambi. [Basi hali hii ndiyo iliyotajwa hapa kuhusiana na wanafiki, kwamba udhuru wao haukubaliki, na kwamba zimekwisha thibiti hali zao mbovu na matendo yao mabaya.] Na ima waadhibiwe kwa adhabu na kutiwa adabu halisi juu ya dhambi zao. Na ima waachiliwe mbali wala wasikumbwe na adhabu ya kweli kwa yale waliyoyatenda. Na hali hii ya tatu ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu aliamrisha kuhusiana na wanafiki, na ndiyo maana akasema: "Watawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali;” yaani, msiwakemee, wala msiwapige viboko, wala msiwauwe. “Hakika hao ni najisi;” yaani, hakika wao ni wachafu na waovu. Hawastahiki kujaliwa, wala karipio na adhabu haviwafai kitu. "Na" inawatosha adhabu ya "Jahannam kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.”