التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَأَوْلَـٰدُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَـٰفِرُونَ ٨٥
{85} Yaani, usidanganyike na yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika dunia hii miongoni mwa mali na watoto. Kwa maana hilo siyo kwa sababu ya utukufu wao kwake, bali huko ni kuwadunisha kwake. "Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwazo katika dunia hii," kwa kutaabika katika kuipata, na kuhofu kutoweka kwake, wala hawaifurahii, bali hawataacha kupata taabu na dhiki kwa sababu yake, na itawashughulisha kando na Mwenyezi Mungu na Nyumba ya Akhera mpaka waondoke katika dunia, "na nafsi zao zitoke hali ya kuwa ni makafiri;" kwa sababu mapenzi yao juu yake yaliwanyang'anya yakawatoa kwa kila kitu. Kwa hivyo wakafa hali ya kuwa nyoyo zao zimefungamana nazo, na nyoyo zao zimechomeka kwa sababu yake.