انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٧

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِى قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُۥ بِمَآ أَخْلَفُوا۟ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا۟ يَكْذِبُونَ ٧٧

{77} Basi wakati hawakutimiza yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu, akawaadhibu na "akawafuatisha unafiki katika nyoyo zao" utakaoendelea "mpaka Siku watakapokutana naye, kwa sababu ya kuwa walimvunjia Mwenyezi Mungu yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uwongo." Basi na Waumini wajihadhari na sifa hii mbaya ya kumuahidi Mola wake Mlezi ikiwa atapata makusudio yake fulani, basi bila shaka atafanya hivi na hivi, kisha hatimizi hilo. Kwa maana pengine Mwenyezi Mungu akamuadhibu kwa unafiki wake huo kama alivyowaadhibu hawa. Na Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - alisema katika hadithi iliyothibiti katika 'Sahih Mbili,' “Alama za mnafiki ni tatu: anaposema, husema uongo, na anapofanya agano, anafanya hiana, na anapoahidi, anavunja ahadi." Basi mnafiki huyu ambaye alimuahidi Mwenyezi Mungu na akafanya agano naye kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu atampa katika fadhila yake, hapana shaka atatoa sadaka, na atakuwa katika waliotengenea, alizungumza, lakini akasema uongo, na akafunga agano, lakini [akafanya] uhaini, na ahadi, lakini akaivunja ahadi hiyo.