التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدًا فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ ٱلْخِزْىُ ٱلْعَظِيمُ ٦٣
{63} Huu ni upinzani kwa Mwenyezi Mungu na uasi dhidi yake. Na Mwenyezi Mungu alimuahidi adhabu mwenye kumpinga kwa kauli yake, "Je, hawajui ya kwamba anayempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake?" Kwa kuwa katika upande ulio mbali na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa kuzembea juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu na akayafanyia ujasiri maharamisho yake, "basi huyo hakika ana Moto wa Jahannamu adumu humo?" Na "hiyo ndiyo hizaya kubwa," ambayo hakuna hizaya mbaya zaidi wala ya kutisha zaidi kuliko hiyo. Kwani walikosa neema ya milele, na wakapata adhabu ya Jahiim. Na tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hali yao hiyo.