التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَوْ خَرَجُوا۟ فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا۟ خِلَـٰلَكُمْ يَبْغُونَكُمُ ٱلْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّـٰعُونَ لَهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ ٤٧
{47} Kisha akataja hekima katika hayo, akasema: "Lau wangelitoka kati yenu, wasingeliwazidisha isipokuwa mchafuko." Yaani, upungufu, "na wangetangatanga kati yenu;" yaani, wangewania katika kutia fitina na uovu baina yenu na wangegawanya kundi lenu lililokusanyika pamoja "wakiwatakia fitina." Yaani, wana hima kubwa ya kuwatilia fitina na kuwekea uadui baina yenu, "Na miongoni mwenu" kuna watu madhaifu wa akili "wanaowasikiliza sana." Yaani, wanaitikia wito wao na wanadanganyika nao. Kwa hivyo, ikiwa wana hima kubwa ya kuwaangusha, na kuwatilia uovu kati yenu, na kuwazuia dhidi ya maadui zenu, na wapo miongoni mwenu wale wanaokubali kutoka kwao na kutaka ushauri wao, mnaonaje uovu utakaotokea katika kutoka kwao pamoja na Waumini na hasara yao kubwa? Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ana hekima kamili zaidi alipowakatisha tamaa na kuwazuia kutoka pamoja na waja wake Waumini kwa ajili ya kuwarehemu na kuwafanyia upole ndiyo wasiingiliwe na kisichowanufaisha, bali kinawadhuru. "Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu" na anawafundisha waja wake jinsi ya kujitahadharisha nao, na anawabainishia maovu yanayotokana na kuchanganyika nao.