انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤١

ٱنفِرُوا۟ خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ٤١

{41} Yeye Mtukufu anawaambia waja wake Waumini huku akiwahimiza kutoka kwenda katika njia yake, kwa hivyo akasema: "Tokeni muende mkiwa wepesi na wazito" katika dhiki na raha, katika hali ya na nguvu na katika hali ya kutopenda, katika joto na baridi, na katika hali zote, "na piganeni Jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu." Yaani, fanyeni bidii yenu katika hilo, na tumieni uwezo wenu wote katika mali na nafsi. Na katika hili kuna ushahidi kwamba kama ilivyo wajibu kufanya jihadi kwa nafsi, na pia ni wajibu kufanya [jihadi] kwa mali wakati haja inataka hivyo na ikaitia kwa hilo. Kisha akasema, "Hayo ni heri kwenu ikiwa mnajua." Yaani, kufanya Jihad kwa nafsi na mali ni bora kwenu kuliko kuyaacha hayo. Kwa sababu, ndani yake kuna ridha ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kupata vyeo vya juu Kwake, na nusura ya dini ya Mwenyezi Mungu, na kuingia miongoni mwa majeshi wake na kundi lake.