التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ ٣٣
{33} Kisha Yeye Mtukufu akabainisha Nuru hii, ambayo alikwisha chukua jukumu la kuikamilisha na kuihifadhi. Kwa hivyo akasema, "Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu" ambayo ni elimu yenye manufaa, "na Dini ya haki" ambayo ni matendo mema. Kwa hivyo yakawa yale Mwenyezi Mungu alimtuma nayo Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - yanajumuisha kubainisha haki kutokana na batili katika majina ya Mwenyezi Mungu, na sifa zake, na vitendo vyake, na katika hukumu zake na habari zake, na kuamrisha kila masilahi yenye kunufaisha mioyo, na roho, na miili kama vile kumpwekeshea Dini Mwenyezi Mungu peke yake, na kumpenda Mwenyezi Mungu na kumwabudu, na kuamrisha tabia njema, na maadili, na matendo mema, na adabu zenye kunufaisha, na kukataza yote yaliyo kinyume na hayo, na yenye kupingana nayo miongoni mwa tabia na matendo mabaya, yenye kudhuru mioyo, na miili, na dunia hii, na Akhera. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamtuma na uwongofu na dini ya haki, "ili aipe ushindi juu ya dini zote, hata washirikina wakichukia." Yaani, aiweke juu ya dini zote, kwa hoja na ushahidi, na upanga, na vita, hata kama washirikina watachukia hilo, na wakaitakia uharibifu, wakaipangia njama, basi hakika njama mbaya haidhuru isipokuwa mwenyewe. Kwa hivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itimizwe, na kile alichokichukulia dhamana ni lazima akifanye.