انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٦

ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْكَـٰفِرِينَ ٢٦

{26} "Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini." Na utulivu ni kile ambacho Mwenyezi Mungu hutia katika nyoyo wakati wa wasiwasi, na mtetemeko na mambo ya kutisha kinachozipa uthabiti na kuzituliza, na anazifanya kutua. Nao ni katika neema kubwa za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, "Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona" nao ni malaika. Mwenyezi Mungu aliwateremsha kama msaada kwa Waislamu siku ya Hunain ili wawaimarishe na wawabashirie nusura "na akawaadhibu wale waliokufuru" kwa kushindwa, na kuuawa, na Waislamu kuwateka wanawake wao, na wana wao, na mali zao. "Na hayo ndiyo malipo ya makafiri." Mwenyezi Mungu anawaadhibu katika dunia hii, kisha atawarudisha Akhera katika adhabu nzito.