التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَٰنٍ وَجَنَّـٰتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ ٢١
{21} "Mola wao Mlezi anawabashiria" kwa rehema kutoka kwake, na ukarimu, na wema juu yao, na kuwajali, na upendo juu yao; "rehema zitokazo kwake" alizowaondolea kwazo maovu, na akawafikishia kwazo kila heri, "na radhi" kutoka kwake Yeye Mtukufu juu yao, ambayo ndiyo neema ya kubwa zaidi ya Peponi na tukufu yake zaidi. Kwa hivyo, atawapa radhi zake, na wala hatawakasirikia abadani "na Bustani ambazo humo wana neema za kudumu." Miongoni mwa kila nafsi zinatamani na macho yanafurahia miongoni mwa yale ambayo hajui sifa yake na kiwango chake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, ambayo miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaandalia wale wanaofanya jihadi katika njia yake daraja mia moja, kati ya kila daraja mbili ni kama kati ya Mbingu na Ardhi, na kama viumbe vyote vingekusanyika katika daraja moja tu miongoni mwake, basi lingewatosha wote.