التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِۦٓ إِيمَـٰنًا ۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَزَادَتْهُمْ إِيمَـٰنًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ١٢٤
{124} Yeye Mtukufu Anasema akibainisha hali ya wanafiki na hali ya Waumini inapoteremka Qur'ani, na utofauti uliopo baina ya makundi mawili haya. Akasema: "Na inapokwisha teremshwa Sura” yenye maamrisho na makatazo ndani yake, na habari kuhusu nafsi yake tukufu na kuhusu mambo ya ghaibu na kuhimiza juu ya jihadi; "basi wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani?“ Yaani, wanaulizwa wale waliopata imani kwa sababu yake miongoni mwa makundi haya mawili. Amesema Yeye Mtukufu akibainisha hali halisi: "Ama wale walioamini iliwazidishia Imani” kwa kuijua, na kuifahamu, na kuiitakidi, na kuifanyia kazi, na kuwa na utashi wa kutenda heri na kujiepusha na kufanya maovu. "Nao wanafurahi;" yaani, wanapeana bishara wao kwa wao kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwayo miongoni mwa ishara zake, na kuwawezesha kuifahamu na kuifanyia kazi. Na hili linaashiria kufunguka kwa vifua vyao juu ya ishara za Mwenyezi Mungu, utulivu wa nyoyo zao, na wepesi wa kufuata kwao yake inayowahimiza sura hiyo juu yake.