التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ١٢١
{121} Kisha akasema: "Wala hawatoi masurufu madogo wala makubwa, wala hawalivuki bonde” katika kuwaendea adui yao, “isipokuwa huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.” Na miongoni mwake ni matendo haya ikiwa watamkusudia Mwenyezi Mungu peke yake ndani yake, na wakamsafishia hali katika hilo. Basi katika aya hizi kuna kutia moyo kukubwa na kuhamasisha kukubwa kwa nafsi juu ya kutoka kwenda katika jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kutarajia malipo juu ya magumu yanayowapata katika hilo, na kwamba hilo litawapandisha daraja, na kwamba athari zinazotokana na matendo ya mja analipwa malipo makubwa.