التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَكُونُوا۟ مَعَ ٱلصَّـٰدِقِينَ ١١٩
{119} Yaani: "Enyi mlioamini" Mwenyezi Mungu na katika aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuyaamini! Fanya kulingana na matakwa ya imani yenu, ambayo ni kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kujiepusha na yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu na kujiweka mbali nayo. "Na kuweni pamoja na wakweli” katika kauli zao, vitendo vyao, na hali zao, ambao maneno yao ni ya ukweli, na matendo yao na hali zao haziwi isipokuwa za ukweli tu, zisizokuwa na uvivu na udhaifu, zilizosalimika kutokana na makusudio mabaya, zenye ikhlas na nia njema. Kwani ukweli unaongoza hadi kwenye haki, nao wema unaongoza hadi kwenye Pepo. Yeye Mtukufu Amesema: "Hii ndiyo Siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao...“ hadi mwisho wa Aya.