انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠١

وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ مُنَـٰفِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا۟ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ ١٠١

{101} Yeye Mtukufu Anasema: "Na katika mabedui walio jirani zenu kuna wanafiki; na katika wakazi wa Madina” pia wapo wanafiki "wale waliobobea katika unafiki." Yaani, waliuzoea [na wakaendelea], na wakazidi kuvuka mipaka katika hilo. "Wewe huwajui" kila mmoja wao ili uwaadhibu au uamiliane nao kulingana na unafiki wao. Kwa sababu ya hekima ya ajabu ya mwenyezi Mungu katika hilo. "Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili.” Inawezekana kwamba uwili hapa unamaanisha uwili, na kwamba adhabu yao ni adhabu ya duniani na adhabu ya Akhera. Duniani ni yale yanayowapata miongoni mwa wasiwasi mkubwa, na dhiki, na chuki juu ya yale wanayoyapata Waumini ya ushindi na nusura. Na katika Akhera ni adhabu ya Moto, na ndipo pa kutulia pabaya zaidi. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni kwamba tutawafanyia adhabu kuwa kali mno, na kuwazidishia, na kuirudia.