انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفجر
السورة ٨٩

الفجر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢١–٢٤

كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ٢١ وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ٢٢ وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ ٢٣ يَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى ٢٤

{21 - 24} "Sivyo hivyo!" Yaani, si mali zote mlizozipenda na starehe mlizoshindania zitabaki pamoja nanyi. Bali mbele yenu iko siku kuu na ya kutisha ambayo ardhi na milima na vyote vilivyomo vitateketezwa mpaka vifanywe kuwa tambarare, uwanda, usiokwa na mdidimio wala mwinuko. Na Mwenyezi Mungu atakuja kuhukumu baina ya waja wake katika vivuli vya mawingu, na watakuja Malaika watukufu wakazi wa mbinguni wote "safu safu." Kila mbingu watawajia Malaika wake safu safu wakiwazunguka wasiokuwa wao chini miongoni mwa viumbe. Na safu hizi ni safu za kunyenyekea na kumdhalilikia Mfalme, afanyaye atakavyo. "Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo" malaika wakiivuruta kwa minyororo. Kwa hivyo, mambo haya yakishatokea, basi "siku hiyo mtu atakumbuka" mema na maovu aliyoyatanguliza. "Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?" Kwani wakati wake utakuwa umeshapita, "atasema" akijuta kwa yale aliyoyapuuza upande wa Mwenyezi Mungu: "Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu" ya kubakia milele - matendo mema. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume! Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki!" Na katika hili kuna ushahidi kwamba maisha ambayo mtu anapaswa kujitahidi kuyakamilisha, kuyapata na kutimiza raha zake ni maisha ya nyumba ya kudumu milele.