البروج
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْبُرُوجِ ١ وَٱلْيَوْمِ ٱلْمَوْعُودِ ٢ وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ٣
{1 - 3} "Ninaapa kwa mbingu yenye Buruji!" Yaani, yenye mahali pa mashukio ya jua, mwezi, na sayari, ambazo zimepangika sawasawa katika mwendo wake utaratibu na nidhamu kamilifu kabisa, jambo linaloonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu, rehema zake, upana wa elimu yake na hekima yake. "Na kwa siku iliyoahidiwa!" Nayo ni Siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu aliahidi viumbe kuwa atawakusanya ndani yake na atawajumuisha humo wa mwanzo wao na wa mwisho wao na wa mbali wao na wa karibu wao, siku ambayo Mwenyezi Mungu hawezi kubadilisha wala kuvunja ahadi yake. "Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!" Haya yanajumuisha kila mwenye sifa hizi, yaani mwenye kuona, mwenye kuonwa, aliyepo, aliyeletwa. Na kinachokusudiwa na viapo hivi ni ishara zinazong'aa za Mwenyezi Mungu, hekima yake dhahiri, na rehema yake pana iliyoko katika viapo hivi. Na ilisemekana kwamba kinachokusudiwa na viapo hivi ni kauli yake: