انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النازعات
السورة ٧٩

النازعات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٥–٢٥

هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ ١٥ إِذْ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلْوَادِ ٱلْمُقَدَّسِ طُوًى ١٦ ٱذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ ١٧ فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ ١٨ وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ ١٩ فَأَرَىٰهُ ٱلْـَٔايَةَ ٱلْكُبْرَىٰ ٢٠ فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ٢١ ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ٢٢ فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ٢٣ فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلْأَعْلَىٰ ٢٤ فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلْـَٔاخِرَةِ وَٱلْأُولَىٰٓ ٢٥

{15 - 25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "Je! Imekufikia hadithi ya Musa?" Swali hili linahusu jambo kubwa ambalo ni la yakini kutokea kwake. Yaani, je, ilikufikia hadithi yake "Mola wake Mlezi alipomwita katika bonde takatifu la T'uwaa?" Napo ni pale mahali alipozungumza naye Mwenyezi Mungu, akamneemesha kwa utume, na akamtuma kwa ufunuo, na akamteua, na akamwambia: "Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri." Yaani, basi mkamkataze uasi wake, na ushirikina, na uovu wake kwa maneno laini na ya upole, labda atakumbuka au akaogopa. "Umwambie: Je, unapenda kujitakasa?" Yaani, je, hutaki jambo la kusifiwa lililo zuri ambalo watu wenye ufahamu mzuri hushindana ndani yake? Nalo ni kwamba ujitakase kutokana na uchafu wa ukafiri na kuvuka mipaka na kuelekea kwenye imani na matendo mema. "Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi" kwa kukubainishia pahala pa radhi zake na pahala pa ghadhabu yake "upate kumcha" Mwenyezi Mungu utakapojua njia iliyonyooka. Lakini Firauni akakataa yale ambayo Musa alimwitia, "Basi alimwonyesha Ishara kubwa." Nazo zilikuwa aina mbalimbali za ishara kubwa kubwa. "Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhahiri. Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao." Lakini Firauni "aliikadhibisha" haki "na akaasi" amri. "Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi" za kupinga na kupigana na haki. "Akakusanya" askari wake "akanadi. Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa." Kwa hivyo, wakamtii na kukiri batili yake hivyo wakati alipowachezea mchezo huo. "Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo." Yaani, Mwenyezi Mungu aliifanya adhabu yake kuwa ni mwongozo, karipio na ufafanuzi wa adhabu ya dunia na akhera.